Pamoja na Kwamba Umeme bado haujafika katika kijiji hiki cha Kilelema,kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe Mkoani Kigoma,lakini wenyeji wa eneo hili hawapitwi na mambo ya Dunia kwani Libeneke la Digitali linakula mzigo kama kawa,na huu ni Ukumbi wao wa kuangalia mambo mbali mbali zikiwemo taarifa za habari.
Sasa unaingia Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Kibao kinachoonyesha Njia panda.
Njia hii huwa ni nzuri sana,ila kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya nchi ndio iliyopelekea kukatika kwa eneo hili.
Huu ni moja ya Migahawa ya Chakula katika kijiji cha Muhinda,Wilayani Buhigwe.
Pamoja na kwamba wakazi wengi wa jijini Dar sasa wanahangaika huku na kule kuhakikisha wanaingia kwenye Digitali,lakini Digitali katika kijiji hiki cha Muhinda lilianza kitaaaaaaambooooooo.......
Kibanda maalum cha kuchajia simu na kuuza vocha,lakini kwa leo kimefungwa.hivyo huduma hakuna.
Mwanadada na ndizi yake Kichwani.
Moja ya Misikiti ya Kigoma mjini.
Barabara kuu ya Kuingia Kigoma mjini.
Viota kibao Kigoma Mjini.
Kigoma ya sasa sio kama ya zamani,Kigoma ya leo inakuja na vikwangua anga kila kona.
Salon safi kwa kina kaka na kina dada.
Kiepe kama kawa.
kama kawa.
Kilimo kwanza ndio mpango mzima wa mji wa Kigoma kila kona upitayo.
No comments:
Post a Comment