Hili ni daraja la Sukuma lililopo katika barabara kuu inayounganisha vijiji vya wilaya ya Magu mkoani Mwanza.Daraja hili haliko vizuri sana kutokana na miundombinu yake kuharibika,hivyo ni vyema likafanyiwa marekebisho ya haraka kabla ya kutokea kwa madhara.
Mwendesha pikipiki akipita kwenye Daraja hilo huku sehemu ya mbao zilizopo kwenye daraja hilo zikionekana kung'oka kutokana na kuoza kwa mbao hizo.
Mbao zilizong'oka kwenye Daraja hilo zikiwa zimeegeshwa tu,huku mawe yakitumika kuziba mashimo yaliyo wazi kati ya nondo na nondo.hali hii ni ya hatari sana,kwani hata magari pia yanapita kwenye daraja hili.Picha na G-Sengo Blog.
No comments:
Post a Comment