HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 23, 2012

watoto waumwao saratani wachora katuni pamoja na Mdau Nathan Mpangala a.k.a Kijasti Bikozz

Jumamosi, tarehe 22.12.2012, Mchoraji katuni, Nathan Mpangala kwa kushirikiana wachoraji wenzake, familia, ndugu na marafiki atatembelea watoto wanaosumbuliwa na saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ikiwa ni muendelezo wa kazi za kijamii kufuatia Tuzo ya Mchoraji Bora wa katuni 2011 aliyopewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na miaka sita ya Mtukwao maarufu kwa jina la Kibonzo kinachorushwa ITV.

Ziara hiyo ina malengo yafuatayo:

Kuwapatia wagonjwa zawadi mbalimbali.

Kuchora nao pamoja. Kwa kuwa katuni zina zinachekesha, zitawasaidia watoto hao kupunguza uwoga wa mazingira ya hospitali, zitawasahaulisha maumivu na kuwafanya kuwa bize na kufurahia siku yako.

Katika ziara hiyo Mpangala aliambatana na baadhi ya wachoraji katuni na marafiki wa Programu ya Wafanye Watabasamu na kuwapa zawadi watoto zawadi mbali kisha wakapata nafasi ya kuchora nao michoro ya kawaidha na ile ihusuyo maisha yao ya kila siku hospitalini hapo.

Kwa niaba ya watoto, Mpangala anaishukuru familia yake, ndugu na marafiki wa Programu ya Wafanye Watabasabu kwa zawadi mbalimbali walizochangia ambazo zimefanya ziara hiyo kuwa ya mafanikio.

Pia anashukuru wachoraji wote waliojitokeza na kuungana naye Muhimbili kwani uwepo wao ulirahisisha usimamiaji wa zoezi la uchorajikwani kila mtoto alisikilizwa pale alipohitaji maelekezo hivyo kufanya watoto.
Matukio mbalimbali ya yaadhi ya watoto wanaendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, wakijimwayamwaya kwa kuchora wakati walipotembelewa na mchoraji katuni, Nathan Mpangala kupitia program yake ya Wafanye Watabasamu ambapo pia aliambatana na baadhi ya wachoraji katuni, ndugu na marafiki wa Wafanye Watabasamu, jana.
Mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa Chanel 10, Bi. Hoyc Temu, akipata maelekezo ya kitaalam ya jinsi ya kuchora toka kwa mmoja wa watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, jana. Matukio ya ziara hiyo yatarushwa na kipindi hiko hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad