Maandamano ya Kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani yakipita mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipata maelezo kuhusu Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kutoka kwa Afisa wa TTCL mkoani Lindi,Bi. Anifa Chingumbe wakati alipokuwa akitembelea Mabanda mbali mbali ya Maonyesho yaliyokuwepo kwenye uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi jana,ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Lindi wakiwa wamejazana kwenye Banda la TTCL ili kupatiwa maelezo mbali mbali juu ya mambo ya Mawasiliano.
Meneja Biashara wa TTCL Mkoa wa Lindi,Bw. Omari Mbogo akipokea cheti cha ushiriki kwenye Maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani,kutoka kwa mmoja wa waratibu wa maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Ludovick Mwananzila.
wafanyakazi wa TTCL Mkoani wakiwa katika picha ya pamoja kwenye maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment