HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 5, 2012

Tamthilia ya "SIRI YA MTUNGI" yazinduliwa rasmi leo

Tamthilia mpya kabisa ya Televisheni kutoka kwa Watu wa Marekani! Onyesho la Kwanza la SIRI YA MTUNGI litakuwa ITV saa 3.30 usiku tarehe 9 Desemba. Na EATV saa 3.30 usiku tarehe 12 Desemba.

Mchanganyiko mzuri wa wahusika wa Siri ya Mtungi, waliohusiana kwa damu au ndoa,  au kwa mapenzi tu, unaunda jamii inayohamasishwa na penzi, lililoletwa na woga, ushirikina na usaliti, ikinyanyuliwa na ucheshi na furaha, na kupewa nguvu ya mshikamano wa ndani wa familia na urafiki.

Tamthilia hii ya Televisheni ni Programu ya awali ya TCCP (Tanzania Communications  Capacity Project) iliyotekelezwa na JHU-­‐CCP (Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communications Programs) kwa msaada wa USAID (United States Agency for International Development) na kama sehemu ya PEPFAR (US President’s Emergency Fund for AIDS Relief).

Ikiwa imetayarishwa na MFDI (Media For Development International), Siri ya Mtungi inawaleta pamoja Wasanii bora wa Tanzania, waandishi, wana mitindo ya nguo, wakurugenzi wa sanaa, waigizaji na watendaji wa filamu kwenye mafanikio makubwa ya ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni Tanzania.

Kati ya mitaa yenye harakati nyingi ya Dar es Salaam na ile iliyo kimya ya Bagamoyo, tunapenya nyuma ya milango iliyofungwa mpaka kwenye maisha ya Cheche na mkewe Cheusi, binti wa kiongozi maarufu katika jamii, mwenye wake wengi, Mzee Kizito, pamoja na wahusika wengine kama Duma, mwana DJ; Lulu-­‐ shangingi lililokubuhu; Farida-­‐ roho ya nyoka; Masharubu-­‐ mzee kikwekwe na wengine wengi.

RATIBA YA ITV: Jumapili 3.30 usiku -­‐ Jumatano 3.30 usiku
 RATIBA YA EATV: Jumatano 10.30 Alasiri -­‐ Alhamisi 7.00 Mchana -­‐ Jumamosi 10.30  Alasiri

Mtengenezaji wa Tamthilia hiyo ya Siri ya Mtungi,John Riber akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi Tamthilia hiyo itakayokuwa ikirushwa na kipindi cha Televisheni cha ITV.
Baadhi ya washiriki wa Tamthilia hiyo wakiwa kwenye picha ya Pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad