HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 22, 2012

Taifa Stars yaitumia vyema mechi ya Kirafiki,Yaichapa Zambia bao 1-0

 Hivi ndivyo Ulivyosomeka Ubao wa Matokeo katika Uwanja huu wa Taifa jijini Dar es Salaam,ambapo matokeo haya yalikuwa hivi mpaka mwisho wa mchezo uliomalizika hivi punge kwenye uwanja wa Taifa.Taifa Stars imeshinda bao 1-0.
 Mshambuliaji wa Taifa Stars,Mrisho Ngassa akijiandaa kuachia shuti kali lililoipatia  Stars bao la kuongoza wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda bao 1-0.
 Mshambuliaji wa Taifa Stars,Hamis Mcha (katikati) akiwachachafya mabeki wa timu ya Zambia katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa stars imeshinda bao 1-0.
 Hamis Mcha (7) akiendelea kuwapa kazi mabeki wa timu ya Zambia.
 Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akiingia kwenye lango la timu ya Taifa Stas,huku beki wa Stars,Aggrey Moris akijiandaa kukabiliana nae.
 Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akijaribu kutaka kumtoka beki wa Taifa stars,Salum Aboubakar wakati wa Mchezo wa Kirafiki uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Taifa stars imeshinda kwa bao moja lililotiwa kimiani na Mshambuliaji machachari,Mrisho Ngassa mnamo dakika ya 45 ya mchezo. 
 Kocha wa Taifa Stars,Kim Poulsen akipeana mkoni na Kocha wa Zambia ambaye alionekana kutofurahishwa na Matokeo ya kufungwa kwa Timu yake,mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar jioni hii.Taifa Stars imeshinda bao 1-0.
Kocha wa Zambia hataki kumsikiliza mtu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad