MAMA LUCY ADAM SAMILLAH
Familia ya Marehemu Mama Lucy Adam Samillah wa Arusha, inapenda kuwashukuru wote walioshiriki katika kumuuguza,kifo,msiba na hatimaye mazishi ya marehemu mama yetu mpendwa, aliyefariki tarehe 26 Oktoba na kuzikwa tarehe 31 Oktoba 2012 mkoani Arusha.
Shukrani za pekee zimwendee Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete,Waziri Mkuu,Mhe. Mizengo Pinda na mkewe mama Tunu Pinda,Watumishi wote wa Ikulu,kuanzia Mnikulu Mkuu na watunza nyumba wote wa Ikulu zote nchini.
Shukrani pia ziufikie uongozi wa mkoa wa Arusha,kuanzia Mkuu wa Mkoa na watumishi wanzake wote wa ofisi yake kwa msaada wao katika kipindi chote.
Shukrani za pekee pia ziwaendee madaktari wote na wauguzi wote wa hospitali alizotibiwa marehemu na zile walizompatia huduma katika kipindi chote cha ugonjwa wake mpaka mauti yalipomkuta.
Tunawashukuru pia ndugu wote,jamaa,marafiki na majirani kwa msaada wao wa hali na mali katika kipindi hiki chote.
Ni vigumu kumshukuru kila mtu mmoja mmoja, hivyo basi tunawaomba wote mpokee shukrani zetu za dhati, na tunasema asanteni sana na Mungu awabariki.
Familia inapenda kuwaalika katika Ibada ya Arobaini na Shukrani ya marehemu itakayofanyika Nyumbani kwake Haile Selassie Road, Arusha siku ya Jumamosi tarehe 8 Desemba 2012 kuanzia saa 4 Asubuhi.
Asanteni na Karibuni sana
Raha ya Milele Umpe Ee Bwaba na Mwanga wa Milele Umwangazie Apumzike kwa Amani.
Amina
No comments:
Post a Comment