Redd's Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred, ambaye yupo mjini Bukoba akikabidhi sehemu ya misaada kwa Wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Msingi,Mugeza Mseto wakati alipotembelea Shule hiyo ambayo ni maalum kwa watoto wenye ulemavu ya Mugeza Mseto, inayofundisha wanafunzi wenye ulemavu.Miss Tanzania huyo pia alitembelea Kituo cha Nusura ambacho kinatunza watoto yatima kilichopo eneo la Kashai.
Mrembo Brigitte Alfred, ambaye pia ni Balozi wa Walemavu wa ngozi, (Albinos) ametoa misaada ya kijamii katika vituo hivyo. Vifaa hivyo ni pamoja na Fimbo maalum za kutembelea walemavu wasioona, Miwani, Kofia na Madawa ya ngozi kwa ajili ya Walemavu wa ngozi. Pamoja na vyakula.
Kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam,Redd's Miss Tanzania 2012 ataelekea Mwanza kwa shughuli zingine za kijamii.
Redd's Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred (katikati) akikabidhi mafuta maalu ya kupaka watu wenye ulemavu wa Ngozi,kwa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo.Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania,Albert Makoye.
Mmoja wa Watoto waosoma katika shule ya Mugeza Mseto iliopo mjini Bukoba ambaye ni Mlemavu wa Macho akipokea fimbo maalum ya kutembelea.
Redd's Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred akiwa amembeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi anaeleleka katika kituo cha Kituo cha Nusura ambacho kinatunza watoto yatima kilichopo eneo la Kashai,mjini Bukoba.Kulia ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania,Albert Makoye.
Redd's Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma kwenye shule ya Mugeza Mseto iliopo mjini Bukoba.
Baadhi ya Walimu wa shule ya Mugeza Mseto wakiwa pamoja na Redd's Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred.Picha na Bukoba Blog.
No comments:
Post a Comment