Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.
Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa kumsaidia matibabu,alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.(picha na Freddy Maro)
woiye kwa mungu kuna kila aina ya baraka kwangu ni amtafute mungu xaxa
ReplyDeleteray c hope now you have seen how the world look like its your time now to make a decision search for God now you are still young
ReplyDeleteray c hope now you an experience how the world look like its your time to make decision search for God mrembo
ReplyDelete