Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Jaji Kiongozi Fakhi Jundu (kushoto),Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe (watatu kulia) na mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo lililojengwa kwa nguvu za wananchi na wafadhili katika kata ya Rondo,jimbo la Mtama,Lindi vijijini leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Jaji Kiongozi Fakhi Jundu wakikagua jengo jipya la mahakama ya Mwanzo lililojengwa kwa nguvu ya wananchi na wafadhili mbalimbali katika kata ya Rondo, jimbo la Mtama,Lindi vijijini leo.(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mlemavu aliyetambulika kwa jina la Mwendo Saidi ,mkazi wa Lindi Vijijini.Rais Kikwete ameahidi kumpatia Msaada wa Bajaji mlemavu huyo,itakayomuwezesha kufanya shughuli zake mbali mbali.
No comments:
Post a Comment