HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 1, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AWASILI MKOANI LINDI TAYARI KWA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika uwanja wa ndege wa Lindi mara baada ya kuwasili mkoani Lindi asubuhi hii ambako anahudhuria maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yanayofanyika Kitaifa kwenye uwanja wa Ilulu mkoani humo, wadau mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi wamejitokeza na kushiriki katika maonyesho hayo yenye lengo la kuelimisha na kukumbusha juu ya hatari za ugonjwa wa ukimwi na mbinu mbalimbali za kupambana nao.Watatu kulia ni Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Lindi,Mh. Ludovick Mwananzila.Kauli mbiu ya mwaka huu ni
"Tanzania Bila Maambukizi mapya, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi Inawezekana".
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Hussein Mwinyi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi Mkoani.katikati ni Mh. William Lukuvi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera na uratibu wa bunge
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Lindi mjini,Mh. Salum Barwany wakati alipowasili mjini Lindi asubuhi hii kwenye uwanja wa ndege wa Lindi.
Viongozi mbalimbali wakimlaki Rais Jakaya Kikwete kwenye uwanja wa ndege wa Lindi leo asubuhi hii.PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad