




Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Festo Chonyo akitambulisha viongozi na watumishi walioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwenye ziara yake kwa wananchi wa kata ya Matanga katika Manispaa ya Sumbawanga.
Afisa kilimo Manispaa ya Sumbawanga Ndugu George Lupilya akisoma taarifa ya maendeleo ya kilimo katika Manispaa ya Sumbawanga kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injnia Stella Manyanya (Hayuko pichani)
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi waliojitokeza kumsikiliza katika kata ya Matanga leo.

Barabara mpya ya lami ya Sumbawanga- Matai- Kasanga inayoendelea kujengwa, Msafara wa Mkuu wa Mkoa ukipita kuelekea kata ya Matanga ukitokea Mjini Sumbawanga. Hakika ujenzi wa barabara hii unakwenda kwa kasi inayoridhisha kwa sasa. Picha na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa-rukwareview.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment