Rais wa bendi ya FM Academia Bw. Nyoshi El Saadat na waliokuwa wakurugenzi wa bendi hiyo miaka ya nyuma Abas Mwinyi Sadamu Hussein kushoto na Felician Chaula kulia kwa Nyoshi El Saadat pamoja na warembo mashabiki wa bendi ya FM Academia wakikata keki kwa pamoja, wakati sherehe ya Bendi hiyo kutimiza miaka 15 ya huduma yake katika kutoa Burudani nchini Tanzania, iliyofanyika kwenye klabu ya Msasani jijini na kuambatana na onyesho kubwa na la kukata na shoka lililoshirikisha Mashabiki, Wadau na watu wa karibu na bendi hiyo.
Onesho la bendi ya FM Academia kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini linadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo. PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM
Wakurugenzi wa bendi hiyo miaka ya nyuma Abas Mwinyi Sadamu Hussein kushoto na Felician Chaula suti nyeusi wakifungua shampeni wakati wa hafla hiyo.
Hii ndiyo keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya hafla hiyo
Mwanamuziki Jose Mara wa bendi ya Mapacha Watatu ambaye pia aliwahi kuwa mwanamuziki wa bendi ya FM Academia akifanya vitu vyake na bendi yake.
Hapa mzuka wa muziki umepanda na uko juu sana kama unavyoona.
No comments:
Post a Comment