HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 6, 2012

ECASJA yafufuliwa, Somoe Ng'itu aula

Na Mwandishi Wetu, Kampala 

MWANDISHI mwandamizi wa michezo wa gazeti la NIPASHE, Somoe Ng'itu, hivi karibuni alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (Wanawake) ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo wa Afrika Mashariki na Kati (ECASJA).

 Somoe alishinda nafasi hiyo baada ya kupata kura nne kati ya saba ambapo alimshinda mwandishi, Lydia Namakula wa New Vision ya Uganda huku Katibu Mkuu wa zamani wa TASWA, Abdul Mohamed alichaguliwa kuwa Mweka Hazina. 

Katika uchaguzi huo uliowahusisha waandishi mbalimbali wa habari za michezo kutoka katika ukanda wa CECAFA ambao wako jijini hapa wakiripoti mashindano ya Kombe la Chalenji yanayoendelea jijini Kampala, Mark Namanya, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo wa Uganda (USPA), alichaguliwa kuwa mwenyekiti. 

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilichukuliwa na Bonnie Mugabe wa Rwanda, Mike Okinyi (Katibu Mkuu). Wajumbe wengine waliochaguliwa katika chama hicho ambapo watakaa kwa muda wa mwaka mmoja madarakani ni pamoja na Desire Hatugimana (Burundi), Patrick Kanyamozi (Uganda). 

Moja ya malengo ya chama hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1982 lakini kilikufa ni kuendeleza taaluma ya waandishi wa michezo katika ukanda wa CECAFA na kukuza michezo yote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad