HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 26, 2012

DIAMOND, DIMPOZ WAFANYA KUFURU USIKU WA X-MAS DAR LIVE

...Leka dutigite: Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Diamond wakiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa Leka dutigite.
Ommy Dimpoz 'on da stage'!
Dimpoz na wasanii wake wakiwasha moto kuwakumbuka wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki.
...Dimpooo...zzz: Umati ukipiga yowe wakati Ommy Dimpoz akifanya kufuru stejini.
...Platnumz hewani: Diamond akiwa amebebwa juu na madansa wake.
...Nataka kulewa, lewa...: Diamond akiimba wimbo wake wa Nataka Kulewa.
...Nature ua... Nature ua... Nature ua..: Ndivyo Juma Nature alivyokuwa akienda sambamba kwa staili hiyo na mashabiki.
...Wanaume Halisi wakiendeleza libeneke ndani ya Dar Live.
Vanessa Mdee akipelekeshana puta na Dimpoz stejini.
...Zitto kazini: Siyo siasa tu, hata mistari mi mkali.
Kikosi cha Diamond Platnumz kazini.
Dimpoz na Vanessa Mdee wakimwaga nyuki stejini.
Manjonjo ya madansa wa Dimpoz.
Diamond akiwachizisha mashabiki.
Madansa wa Dimpoz wakionyesha umahiri wao.
...Wakizidi kukonga nyoyo za mashabiki.
Zitto Kabwe akicheza kwenye kiti baada ya kunogeshwa na swagga za Dar Live.
Shughuli pevu ya Diamond na madansa wake.
...Waacheni watoto waje kwangu: Ndivyo allivyokuwa akichombeza Diamond wakati akitaka kumchukua mtoto huyu.
Platnumz akiipagawisha meza ya wageni waalikwa.
Waalikwa wakionyesha nyuso za tabasamu wakiongozwa na Mwasiti (wa pili kulia) na Prodyuza aliyetengeneza wimbo wa Leka dutigite, Tudi (wa tatu kushoto).
Prodyuza na Mwanamuziki mkongwe, Ally Mohammed 'Baucha' akikamua stejini.
...Nimpende naniii... Nimpende...: Wapambe "Wemaaaaaaaaaaaaa!"
Madansa wa Extra Bongo wakinogesha zaidi burudani za X-Mas ndani ya Dar Live.
Mpiga gitaa la besi wa Extra Bongo, Hosea Mgoachi akijiachia na shabiki jukwaani.
---
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' na Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' usiku wa kuamkia leo wameweka historia kwa kufanya shoo ya aina yake ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. 

Wasanii hao walisindikizwa na mkali Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi, Msanii mkongwe Ally Baucha pamoja na Bendi ya Extra Bongo. Shoo hii imeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Serengeti Premium Lager na Vodacom - Wajanja wa Kujirusha.

(PICHA ZOTE : RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad