HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 30, 2012

BONANZA LA KUAGA MWAKA LA KLABU ZA JOGGING LAFANA JIJINI DAR LEO.

Vijana wa jiji la Dar es Salaam kutoka kwenye Klabu za Jogging zipatazo 12 wakifanya mazoezi ya aina mbalimbali mapema leo asubuhi jijini Dar es Salaam Kabla ya kuanza kwa Bonanza la kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013 lililoandaliwa na Klabu ya Jogging ya Kawe jijini humo.

Hapa kazi tu!

Vijana wa jiji la Dar es Salaam kutoka kwenye Klabu za Jogging zipatazo 12 wakifanya mazoezi ya kukimbia mapema leo asubuhi jijini Dar es Salaam Kabla ya kuanza kwa Bonanza la kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013 lililoandaliwa na Klabu ya Jogging ya Kawe jijini humo.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Iddi Azzani akiongoza timu yake ya Klabu ya Jogging ya Barafu ya Magomeni wakati wakishangilia ushindi wao.
"Hapa lazima waje..." Mh. Iddi Azzan akishiriki kuvuta kamba.

Katibu wa Kawe Jogging Klabu (Mdau) Razalo Ngimba (katikati) akiwa na Refaree maarufu nchini Othmani kazi (kulia) wakati wa mazoezi kabla ya bonanza kuanza.


Mbunge wa jimbo la Kinondoni Iddi Azzani, akiwapa mazoezi vijana wa Klabu Jogging 12 za maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam  wakati alipoalikwa kushiriki Bonanza la kumaliza mwaka lililoandaliwa na Kawe Jogging Klabu na kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Kabla ya bonanza hilo kulikuwa na mazoezi ya kukimbia umbali wa Kilometa nana kutoka Kawe kupitia Lugalo hadi Mbezi Beach na kurejea kwa kupita barabara ya Bagamoyo ya zamani hadi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad