HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 7, 2012

WASHINDI DROO YA PILI ‘SHINDA NOAH’ WAKABIDHIWA ZAWADI

 
Mkuu wa Chuo cha Zoom Polytechnic, Gaudios Shija (kushoto), akikabidhi zawadi ya kompyuta kwa Rehema R. Saneje.

WASHINDI wa droo ya pili ya shindano la ‘Shinda Noah’ linaloratibiwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Limited, mapema leo wamekabidhiwa zawadi zao walizoshinda katika bahati nasibu hiyo iliyochezeshwa Oktoba 31 mwaka huu kwenye viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam.
Zawadi hizo zimekabidhiwa na mmoja wa wadhamini wa droo hiyo, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Zoom Polytechnic, Gaudios Shija, na Afisa Masoko wa Global Publishers, Benjamin Mwanambuu, katika makao makuu ya ofisi za Global Publishers yaliyopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)

 
Rehema R. Saneje akiwa katika pozi na kompyuta yake muda mfupi baada ya kukabidhiwa.
Afisa Masoko wa Global Publishers, Benjamin Mwanambuu (kushoto), akimkabidhi mshindi wa jezi, Rehema Kigadye.
Mshindi wa simu aina ya Samsung Tablet, Leah Andrew (kulia), akipokea zawadi yake kutoka kwa Mwanambuu.
 
Rukia Vitali akikabidhiwa TV Flat Screen na Mwanambuu.
Washindi wakiwa katika pozi la pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad