Mapema leo asubuhi,Wakaji wa Jiji la Mbeya wameamua kupanga mawe Barabarani katika eneo la Mama John ili waweze kusimamisha magari yote yanayosafirisha mafuta kwenda nchi za jirani na kuweza kuyachukua mafuta hayo kwa ajili ya mahitaji mbali mbali.hali hiyo imekuja kutokana na hali ya uhaba wa Mafuta uliolikumba jiji hilo kwa takribani wiki mbili sasa.
Ilikuwa hakuna gari inayoweza kupita katika eneo hilo kwani Mawe yaliyokuwa yamewekwa yalikuwa ni Makubwa sana.
Ilibibi watumie na utaratibu mwingine wa kupaki malori ya mchanga pembeni ili Magari hayo yasipite.
Wakazi wa Mbeya wakiwa Wamekaa Pembeni na Madumu yao kusubiria Magari hayo yanayosafirisha Mafuta.
Jamaa wakikomaa na Moja Jiwe kuhakikisha linafika Barabarani ili kushinikiza wapate mafuta.
"Hapa ni Mpaka kieleweke leo,kwanini Mafuta yapelekwe nchi jirani na wakati sie hatuna?"haya ndio yalikuwa maneno ya wakazi hawa wa jiji la Mbeya.
Gari la Kampuni ya Uchapishaji wa Magazeti ya Mwananchi likiwa liomekwa katika eneo hilo.
Foleni sio ya mchezo.
Askari Polisi walifika katika eneo hilo Baada ya kusikia hali ni tete,hivyo walitumia busara zao kuwataka watu hao waache mara moja zoezi hilo kwa jambo lao ninashughulikiwa.
Hiki ni kituo cha Mafuta cha Kampuni ya Orxy kilichopo Mama John,jijini Mbeya kikiwa hakiuzi mafuta huku msururu wa magari na pikipiki ukionekana kutokata tamaa.
PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG
PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG
No comments:
Post a Comment