Mkurugenzi wa mafunzo wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Mutahyabarwa Gozibert (katikati) akizindua kitabu cha mwongozo wa utoaji wa huduma bora za afya nchini kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika mkutano uliowahusisha wadau wa afya kutoka maeneo mbalimbali nchini leo jijini Dar es salaam.
Mganga mkuu wa serikali mstaafu Dkt. Gabriel Mpunda akiwasilisha mada kuhusu mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma bora za afya nchini kwa wadau wa afya waliohudhuria mkutano wa taifa wa majadiliano ya utoaji wa huduma Bora za afya leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Hospitali wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Magreth Muhando akizungumza na wadau wa afya kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa niaba ya Katibu mkuu wa wizara hiyo kuhusu hatua zinazochuliwa kuboresha huduma za afya na uboreshaji wa elimu katika vyuo vya sayansi ya afya na tiba wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Wadau wa huduma za afya kutoka maeneo mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa mkutano huo.
Wadau wa huduma za afya kutoka maeneo mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa mafunzo wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Mutahyabarwa Gozibert akiwatoa hofu baadhi ya wadau waliotaka kujua kuhusu ubora wa elimu inayotolewa sasa kwenye kozi ya uuguzi kwa kipindi cha miaka 2 badala ya miaka 4 ya awali. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
No comments:
Post a Comment