HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 19, 2012

Soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya

Hili ndilo soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya ambapo wafanya biashara waliokuwa katika Soko la Mwanjelwa ambalo liliteketea kwa Moto miaka kadhaa iliyopita walihamia katika Soko hili.Hapa ni mie nikitoka sokoni hapo kufanya shopingi ya kiaina.
Nikiendelea kukata Mitaa ndani ya Soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya.
Matunga ya kila aina yanapatikana ndani ya soko hili.
Vitunguu vya kumwaga.
Hata Samaki wa Mafungu pia wanapatikana ndani ya Soko hili
Eneo ni kubwa ndani ya Soko hilo kiasi kwamba hata Baiskeli zinaendeshwa bila shida yeyote.
Vitu vya Yebo Yebo
Eneo la Kuuzia Ndizi.
Ndani ya soko hilo wafanya biashara naona kama wamekugomea vileee,maana sehemu nyingi za ndani ziko wazi kabisa.
Hii ni sehemu ya Biashara ya viatu.
Sagula Sagula kama kawa ndani ya Soko la Sido Mwanjwelwa jijini Mbeya.
Mdau akisubiria wateja.
Hata Sufuria pia zipo ndani ya soko hili.
Za kubani pia zipo.
Kushoto ni jengo jipya la Soko la Mwanjelwa ambalo litafunguliwa siku yeyote kuwanzia sasa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad