HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 20, 2012

SAUTI ZA BUSARA ZANZIBAR KUENDELEA KUMTUNZA BI. KIDUDE

Na Mohammed Mhina, Zanzibar

Kampuni ya Sauti za Busara Zanzibar imesema kuwa haitaachana na Mwimbaji Mkongwe wa Muziki wa Taarabu hapa nchini Bi. Fatuma Bint Mbaraka maarufu kama Bi Kidude hata baada ya kutangaza kutaka kuachana naye.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo inayoendesha Tamasha la kila mwaka la Sauti za Busara visiwani Zanzibar Bw. Yusuf Mahmoud, imesema kuwa kamwe kampuni hiyo haitamtupa Bi. Kidude.

"Wakati tunajuta kwamba baadhi ya watu wanaamini vinginevyo, tunatarajia kutamka na kuthibitisha tena kwamba tunatafuta na kuwafanyia wasanii kutoka Afrika Mashariki, Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla, itaendelea kumsaidia Bi. Kidude maisha yake yote". Imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo taarifa hiyo imeongeza kuwa Busara Promotion iko tayari kuzikabidhi fedha za Bi Kidude kwake mwenyewe ama kwa mtu ambaye atatajwa na Bi. Kidude ili mradi kuwa makabidhiano hayo yatafanyika kisheria yakiwahusisha mashahidi tena wakiwemo mwanasheria, mwakilishi kutoka Serekalini na mbele ya Waandishi wa Habari ili kuepuka utata.

Hivi karibuni, Sauti za Busara iliitisha mkutano na waandishi wa habari Zanzibar ili kuelezea juu ya suala la muimbaji huyo hodari wa nyimbo za utamaduni Bi Kidude ambapo ilitolewa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za mwimbaji huyo zilizokuwa zikihifadhiwa na Sauti za Buisara.

Mkutano huo uliohudhuliwa na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari, uliitishwa kufuatia taarifa za kudhulumiwa kwa fedha kwa Bi Kidude malalamiko ambayo yalikosa kujulikana chanzo chake.

Hata hivyo katika mkutano huo ilibainika kuwa kuna watu walionyuma ya pazia yaani mgongoni mwa Bi Kidude ambao wanamhitaji kwa lengo ls kumtsgfunis frdhs zake kwa kujifanya wasamalia wema.

Waandishi waliitaka Sauti za Busara kuendelea kumlea Bi Kidude na kuachana na maneno ya mitaani ambayo yakishikiwa bango hayatakuwa na tija kwa Bi. Kidude ama wanaojifanya wasamalia wema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad