HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 25, 2012

Rais Kikwete ateta na Rais Kabila jijini Kampala,Uganda

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila mjini Kampala Uganda leo baada ya kumalizika kwa mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa makuu.Mkutano huo ulijadili hali ya usalama ya Mashariki ya DRC eneo ambalo limetekwa na waasi wa kikundi cha M23.Baadaya Rais Kikwete na ujumbe wake walirejea jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere muda mfupi baada ya kuwasili kutokea Kampala,Uganda ambapo alihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa makuu. (picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad