HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 4, 2012

Rais Kikwete aendelea na Ziara Yake jijini Arusha


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua barabara ya Minjingu-Babati-Singida nje kidogo ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara. Anayeshuhudia kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji) Dkt Mary Nagu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakiweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maeneo ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero wakifurahia baada ya kuzindua barabara ya Minjingu-Babati-Singida nje kidogo ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara. Anayeshuhudia kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji) Dkt Mary Nagu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Frederick Sumaye wakati wa mkutano wa hadhara mjini Katesh mkoani Manyara.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akipanda mti kama kumbukumbu baada ya Rais Kikwete kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maene ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakielekea kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maeneo ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Arusha baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maene ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Arusha baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maene ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Sehemu ya barabara ya Minjingu-Babati-Singida iliyozinduliwa na Rais Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mhe Rose Kamili baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji wa Mwakonko Singida Mjini.PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad