Mama wa Mitindo nchini Tanzania, Asia Idarous kupitia Kampuni yake ya Fabak Fashions,leo wanakuletea onyesho kubwa la Khanga za Kale litakalofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Onyesho hili kubwa ambalo limekuwa likifanya vizuri kwa takribani miaka minne sasa na kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania hasa katika nchi ya Marekani, litawakutanisha wabunifu zaidi ya 30 kutoka sehemu mbali mbali ambao nao wataonyesha mavazi yao waliyoyabuni.
Watu Maarufu hapa nchini watapanda jukwaani siku hiyo kuonyesha Mavazi ya Khanga za Kale kutoka kwa Mama wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin ambapo fedha itakayopatikana kutokana na onyesho hilo imepangwa kupelekwa kwenye kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Kulea watu walioathirika na Madawa ya Kulevwa kilichopo Kikale Wilayani Rufiji, Mkoani Pwani.
Mgeni Rasmi katika Onyesho hilo,anatarajiwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Mh. Sophia Simba.
No comments:
Post a Comment