HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 20, 2012

MSIBA NEW YORK, Marekani


Marehemu Jesca Emmanuel

Mhe. Tuvako Manongi, Balozi  wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  kwa majonzi makubwa, anasikitika  kutangaza kifo cha  Jesca Emmanuel  (12), Mtoto wa  Afisa mwenzetu  Bw.  Emmanuel Swere Alfred  na Bi Doto, kilichotokea ghafla siku ya Jumapili 18/11/2012 katika Hospitali ya Mt. Sinai, Queens, New York. Taratibu na mipango ya  kuusafirisha Mwili wa Marehemu Mtoto Jesca kwenda kijijini  Bumbombi- Shirati Tanzania kwa mazishi  zinaendelea kwa usimamizi wa Ubalozi na Familia ya Marehemu.

Taarifa zaidi  zitatolewa na Ubalozi  kuhusu  siku, tarehe na  mahali tutakapomuaga   mpendwa wetu  Jesca Emmanuel.

Raha ya Milele Umpe Eee Bwana, na Mwanga wa Milele Umuangazie apumzike kwa amani. Amina
  
UBALOZI WA TANZANIA  UMOJA WA MATAIFA
 NEW YORK

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad