HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 17, 2012

MKUTANO WA 5 WA WANACHAMA WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI WAFANYIKA MJINI KIGALI RWANDA

Waziri wa Utumishi na Ajira wa Rwanda Mhe. Anastace Murekezi (wa pili kushoto) akimkabidhi Tuzo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhani Dau kwa NSSF kuendesha Mafunzo ya hifadhi ya Jamii kwa wanachama wa Afrika Mashariki. Wakwanza kulia kwa Waziri ni Mwenyekiti wa ECASSA Bi.Angelique Kantengwa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Rwanda Social Security Board (RSSB) na kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Uganda Bw.Richard Byarugaba.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw.William Erio akisikiliza mada kutoka kwa Mwakilishi wa ILO (hayupo picha), kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw.Eliud Sanga.
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka,Mwenyekiti wa Bodi ya PPF,Dkt. Adolf Mkenda na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio wakiangalia ngoma ya Kinyarwanda ambayo haipo kwenye picha ilipotumbuiza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF Dkt. Adolf Mkenda,Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi.Irene Isaka na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhani Dau wakifuatilia kwa Makini hotuba wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 5 wa wanachama wa Mifuko ya hifadhi ya Jamii uliofanyika Rwanda Kigali tarehe 15 mpaka 16 Novemba,2012.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF Crescentius Magori (kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano NSSF Tanzania Bi.Eunice Chiume na mwakilishi kutoka Kenya wakisikiliza mada.
Mawaziri na Manaibu waziri kutoka nchi za Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano wa 5 wa wanachama wa Mifuko ya hifadhi ya jamii uliofanyika Kigali Rwanda kuanzia tarehe 15 mpaka 16 Novemba, 2012 kutoka kushoto waliokaa ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Tanzania Mhe.Dkt Makongoro Mahanga ,Naibu Waziri wa Kazi wa Zambia Mhe.Roland Chitotela,Watatu katikati ni Waziri wa Utumishi na Ajira wa Rwanda ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi kwenye Mkutano Mhe. Anastace Murekezi, Waziri wa Afya wa Uganda Mhe. Kataike Sarah Ndoboli na Mbunge kutoka Uganda anayeshughulikia Wafanyakazi Mhe. Arinaitwe Rwakajara. Nyuma kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Tamisemi wa Tanzania Mhe. Aggrey Mwanri na Waziri wa Michezo na Serikali za Mitaa Kenya Mhe.Dkt Paul Otwoma.
Mawaziri,Manaibu Waziri na Wakurugenzi Wakuu kutoka nchi za Afrika Mashariki wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya Waziri wa Utumishi na Ajira wa Rwanda wa tatu kutoka kushoto Mhe. Anastace Murekezi kufungua rasmi Mkutano wa 5 wa Hifadhi ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad