Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo, Zenno Ngowi akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kufanyika kwa Maonyesho makubwa ya sekta ya nyumba ya Tanzania Homes Expo yanayotarajiwa kufanyika kwa mara ya pili Nchini Tanzania kuanzia tarehe 7 hadi 9 Disemba 2012,kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar.
Maonyesho makubwa ya sekta ya nyumba ya Tanzania Homes Expo yanayotarajiwa kufanyika kwa mara ya pili Nchini Tanzania kuanzia tarehe 7 hadi 9 Disemba 2012. Kwa mara ya kwanza maonyesho ya Tanzania Homes Expo yalifanyika mwezi June na yalifungwa rasmi na Makamu wa Rais Dr Mohammed Gharib Bilal.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo Ndugu Zenno Ngowi aliseme ‘’Upatikani wa makazi ya uhakika na upatikanaji wa masuluhisho ya ujenzi wa nyumba bado umeendelea kuwa changamoto kubwa kwa Watanzania wengi.
Hata hivyo, katika kipindi hiki Nchini Tanzania tumeshuhudia kukua kwa kasi kwa sekta ya nyumba na huduma nyingine za ujenzi katika siku za karibuni. Hata hivyo uwepo wa taarifa sahihi juu ya masuluhisho mbalimbali yahusuyo sekta ya nyumba limekuwa nin tatizo kubwa, upungufu huu ndio ulikuwa msingi Mkuu wa kuanzisha maonyesho ya Tanzania Homes Expo’’.
Zenno aliongeza kusema ‘’Ni jambo la kujipongeza kuona mabenki kadhaa yanatoa mikopo ya nyumba, lakini taarifa za kina namna ya kupata mikopo hii raia wengi hawajui!, Je ni mara ngapi imebidi mtu kusimamia nyumba yake mwenyewe wakati wataalam na macontractor wapo! Je kabla ya kuchagua aina ya nyumba ya kujenga tunajua mambo muhimu ya kuzingatia? Jibu ni hapana’’.
Tanzania Homes Expo, ni maonyesho yenye lengo la kukuza elimu ya umma kuhusu aina mbali mbali za huduma zinazolenga sekta hii muhimu. Lakini pia Tanzania Homes Expo inatoa fursa kwa watoa huduma za sekta ya nyumba kama; mabenki, mikopo, bima, wakandarasi, wachora ramani, makampuni ya nyumba, makampuni ya ulinzi, marembo, vifaa vya ujenzi na mengi yahusuyo sekta ya nyumba kupata nafasi ya kuelezea huduma wanazozitoa.
Tanzania Homes Expo inadhaminiwa na Azania Bank, Clouds FM, TMRC na Brand Works.
Kwa taarifa zaidi au kushiriki tembelea tovuti; www.tanzaniahomesexpo.org au tuma barua pepe info@tanzaniahomesexpo.org
No comments:
Post a Comment