Malkia wa mipasho nchini, Khadija Kopa, kutoka T.O.T akiwapagawisha mashabiki waliohudhuria Mitikisiko ya Pwani Dar Live Jumamosi.
MALKIA wa mipasho nchini, Khadija Kopa, juzi (Jumamosi) alifunika vilivyo katika Tamasha la Mitikisiko ya Pwani lililofanyika ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.
Tamasha hilo lilipambwa na makundi mbalimbali ya taarab yakiwemo Jahazi,
Coastal, TOT na mengineyo. Watangazaji mahiri kutoka Times Radio
wakiongozwa na Gardner G Habash na Khadija Shaibu 'Dida' walinogesha
tamasha hilo na kulifanya liwe la kipekee.
Mzee Yusuf akimchombeza mkewe, Leila Rashid.
Mashabiki waliopanda stejini kumtunza Mzee Yusuf wakijiachia kwa raha zao.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)
No comments:
Post a Comment