Msanii wa kikundi cha ngoma cha
Bujora akichezea nyoka kwa kuingiza kichwa mdomoni wakati wakitumbuiza watu
waliofika kushuhudia mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race)
yaliyofanyika Mwaloni Mkoani Mwanza jana.
DSC_0208Wapiga makasia 15 wakinyosha
makasia yao juu kabla ya kuanza kwa fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi
(Balimi Boat Race) yaliyofanyika jijini Mwanza jana.
Mabingwa wa Mkoa wa Mwanza wa
Mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) timu ya Cheka na Wengi
kutoka Misungwi wakiwasili ufukweni baada ya kuongoza mbio hizo muda wote huku
wanaofuatia wakipishana kwa sekunde tu.
Nahodha wa timu ya Chekanawengi ya
Misungwi Daniel Mugeng'a, akionyesha kitita cha Tsh 900,000 baada ya kukabidhiwa kutokana na kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya
Mitumbwi (Balimi Boat Race) ngazi ya Mkoa jijini Mwanza jana ambapo
washiriki walishindana kuendesha mitumbwi kwa makasia.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia
Tanzania TBL Fimbo Butallah, akimuelekeza jambo Nahodha wa timu ya Wanawake na
Maendeleo ya Misungwi Tabu Daudi, ambao ndio washindi wa kwanza kwa upande
wa wanawake Mkoa wa Mwanza mara baada ya kukabidhiwa zawadi yao ya ushindi wa
kwanza kitita cha shilingi laki saba (700,000).
Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi
ya Balimi (Balimi Boat Race) Mkoani Mwanza upande wa wanawake timu ya
Wanawake na Maendeleo kutoka Misungwi wakiwa hawaamini kama wameweza
kushinda kwa kuwaacha mbali wenzao na kuwa mabingwa wa mkoa huo na
kukabidhiwa jumla ya shilingi laki saba (700,000) kama zawadi ya ushindi wa
kwanza.
Wapiga makasia 15 wakinyosha makasia
yao juu kabla ya kuanza kwa fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi
Boat Race) yaliyofanyika jijini Mwanza jana.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia
Tanzania TBL akiteta jambo na Afisa Utamaduni na Michezo wa Manispaa ya Ilemela
wakati wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race)
Yaliyofanyika jana Mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment