Timu za wapiga makasia za wanawake zikianza mbio hizo za kusaka kitita cha Tsh.700,000 wakati wa mashindano ya mitumbwi ya Balimi ngazi ya Mkoa yaliyofanyika jana Wilayani Musoma Mkoani Mara ambapo washindi watakao wakilisha Mkoa huo ngazi ya Kanda walipatikana.
Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) Mkoani Mara upande wa wanawake timu ya Kisorya wakishangilia ushindi wao huo mara baada ya kuwasili ufukweni kwa kuwaacha mbali wenzao na kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki saba (700,000) kama zawadi ya ushindi wa kwanza.
Mmoja wa majaji wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi akimchukua nahodha wa mtumbwi ulioshika nafasi ya tatu Manyama Pius kutoka eneo la Kisorya kwenye Manispaa ya Mji wa Musoma Mkoani Mara.
Kaimu Katibu Tawala wa Manispaa ya Musoma Rephael Joseph Nyanda, akimkabidhi kitita cha Tsh.900,000 Nahodha wa timu ya Makasia ya Baruti kutoka eneo hilo la Baruti Mashaka Patel, baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya Mitumbwi (Balimi Boat Race) ngazi ya Mkoa Wilayani Musoma Mkoani Mara jana anaeshuhudia kulia ni Meneja wa Mauzo wa Kanda ya Ziwa Endrew Mbwambo.
Nahodha wa timu ya wanawake ya Kisoryan Nyamisi Deo akionyesha kitita cha fedha cha Tsh 700,000 ikiwa ni zawadi kwa mshindi wa kwanza.
Nahodha wa timu iliyoshika nafasi ya kwanza wanaume ya Baruti kutoka eneo hilo la Baruti Mashaka Patel akionyesha kitita cha Tsh.900,000 baada ya kushinda nafasi hiyo nakupata pia nafasi ya kuwakilisha mkoa huo ngazi ya kanda kwenye mashindano yatakayofanyika Mkoani Mwanza Disemba 2 mwaka huu.
Wasanii wa Timu ya Promosheni ya Bia ya Balimi wakiwatumbuiza wananchi mbalimbali waliojitokeza kushuhudia mashindano ya mitumbwi ya Balimi ngazi ya Mkoa yaliyofanyika jana Wilayani Musoma Mkoani Mara.
Timu za wapiga Makasia kwa upande wa wanawake Mkoani Mara zikinyoosha makasia muda mfupi kabla ya kuanza kwa mashindano hayo yaliyofanyika jana Wialayani Musoma ambapo timu ya Wanawake Kutoka Kisoya iliibuka washindi wakwanza na kujizolea kitita cha Tsh.700,000.
Hongera zao akina dada na wamama kazi si ndogo huo ni ujasiri wa hali yajuu.
ReplyDelete