Mshambuliaji wa timu ya Kilimajaro Stars, Simon Msuva (12) akichanja mbuga baada ya kumtoka beki wa timu ya Sudani, Faris Abdallah wakati wa mchezo wa michuano ya Challenge uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela Jijini Kampala,Uganda leo.Kilimajaro Stars imeshinda bao 2-0.
Erasto Nyoni wa Kilimanjaro Stars (4) na beki wa timu ya Sudan, Faris Abdallah wakiwania mpira wakati wa mchezo wa michuano ya Chalenge uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala,Uganda.Kilimajaro Stars imeshinda bao 2-0.
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Mrisho Ngassa akikokota mpira uliozaa goli pili wakati wa mchezo wa Cecafa Challenge 2012 dhidi ya Sudan uliochezwa katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala leo.
Kilimanjaro Stars wakishangilia goli la kwanza lililofungwa na John Bocco wakati wa mchezo dhidi ya Sudan katika michuano ya CECAFA Challenge katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala.
Mashabiki wa timu ya Kilimanjaro Stars waliosafiri kutoka mkoani Kagera wakishangilia baada ya kufungwa kwa goli la kwanza wakati wa mchezo wa Cecafa Challenge 2012 dhidi ya Sudan uliochezwa katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala leo.Kilimajaro Stars imeshinda bao 2-0.
No comments:
Post a Comment