HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 25, 2012

Kilimanjaro Stars Kukipiga leo nchini Uganda

Kipa wa Kilimanjaro Stars, Juma kaseja akitoka Uwanja baada ya
kumalizika kwa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha
Kampala Kampasi ya biashara nchini Uganda jana. Stars inadhaminiwa na
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Edward Christopher akikokota mpira wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara nchini Uganda jana kwa kujianda na mchezo wa michuoano ya Cecafa. 


Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakitoka Uwanjani baada ya kufanya mazoezi katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara nchini Uganda jana. 

Kocha wa Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen amesema ana imani na timu yake itakayotupa karata ya kwanza leo dhidi ya Sudan katika mashindano ya CECAFA Challenge.

Alisema suala la wachezaji  Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kutofika mpaka sasa halimtatizi kwa kuwa ameiandaa timu vizuri na atawatumia wachezaji waliopo. 
 “Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kesho kwa sababu hawajafika lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na wachezaji waliopo,” alisema.

“Nina imani TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,” alisema.

Kuhusu wachezaji kama Aggrey Morris, Mohamed Nassoro na Mwadini Ali kutoka Zanzibar kujiunga na wenzao kuichezea Zanzibar Heroes, Poulsen alisema pengo lao halitampa tatizo kwa kuwa ni changamoto.

“Timu hii  kwa sasa ina wachezaji wengi chipukizi kwa hivyo huu ndio muda wa kuwapima vizuri kwani kwani  haya ni mashindano makubwa,” alisema.
Alisema wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza  dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia ambazo zitacheza leo pia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad