Wachuuzi wa samaki aina ya dagaa
wakisubiri wateja kwenye soko la Mwigobero Wilayani Musoma Mkoani mara
ambapo walieleza blog hii kuwa bei ya dagaa imeshuka kwa asilimia 50 na
zaidi kwa sasa sababu ikielezwa kupungua kwa wateja. Awali bei ya dagaa
hao kwa ndoo moja ikiuzwa kwa Tsh 10,000 lakini sasa inauzwa Tsh 5000
hadi 4000.
Mifuko
ya Plastic (viroba) inayoonekana imesheheni dagaa hao wakiwa tayari
kusafirishwa kwenda maeneo mbalimbali nnje ya Mkoa huo.
Kama ilivyo kwenye mikoa mingi hapa
nchini ni kawaida kukutana na watoto wa umri huu mitaanio wakifanya
shughuli mbalimbali huku wengine wakiomba omba lakini hapa watoto wengi
wapo kwenye ajira hizi za biashara ndogondogo.
MAAJABU YA KAMANGO! Mchuuzi wa
samaki wa Soko la Mwigobero Wilayani Musoma akimkata samaki aina ya
Kamongo huku samaki huyo akiwa hai na akimuepuka kuto mgusa kichwani
kwani pamoja nakuwa amekatwa bado ni mzima na anaweza kukuuma na
kukuathiri. Kwa mujibu wa maelezo ya wachuuzi hao samaki huyo ni mgumu
kufa hata kama akikatwa vipande vyote lakini kichwa kinakua hai kwa
masaa kadhaa bila yakufa na kinaweza kumuuma mtu.
Jengo la Maktaba Kuu ya Mkoa wa Mara
lilipo Wilayani Musoma likiwa kwenye hali mbaya ya uchakavu bila ya
kukarabatiwa huku likiendelea kutumika kwenye mazingira hayohayo
chakavu, baadhi ya maeneo likionyesha kuvuja.
UMEONA TOFAUTI HAPO? Pichani ni
wanafunzi wa shule mbili tofauti, kuna Sekondari na Primary lakini
wanaonekana kufanana kwa umri lakini pia hawa wa Sekondari ndio
waliokuwa wakicheza michezo ya kitoto ya primary kwa kuchota maji taka
na kuwarushia wenzao wa primary ! (Ila wote ni watoto).
No comments:
Post a Comment