Pamoja
na ujenzi mzuri wa kituo hiki cha abiria wavukao kutoka Sengereama kuelekea
Mwanza mjini kwenye Ziwa Victoria, lakini suala la usalama hapa ni ziro kabisa,
magari hayo pichani yakisubiria kivuko lakini hakuna kizuizi chochote
kinachozuia hata kwa dharura kama ikitokea bahati mbayha gari moja kugonga
mwenzake. Lakini hata hivyo hakuna sababu yoyote ya magari haya kusubiri kivuko
kwenye eneo hili la karibu na maji wakati eneo la kutosha lipo
Magari yakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye Kivuko cha Mv
Misungwi, umbali wa kuvuka kwenye eneo hili nitofauti na ule umbali wa
Kigamboni na Posta ambao huchukua dakika tano , hapa ni mwendo wa dakika 20
kufika ng'ambo ya pili.
Tatizo la kuondoa Kivuko kabla ya watu hawajaishi kuingia
nalo hujitokeza maeneo mengi ya vivuko sababu haijulikani, pichani kushoto
mfanyakazi wa kivuko akiondoa kamba iliyofungiwa kivuko kabla ya watu
hawajaisha kuingia na kivuko kimeanza kutoka, nakuwafanya abiria hao kukimbilia
kwa kasi huku wengine wakiwa na watoto wadogo.
Mandhari ya majengo ya kumpumzikia abiria ni nzuri na ni bora zaidi ipo haja ya kuendelea kuimarisha utunzaji wake
Kiwango cha Ubebaji wa mizigo ni Cha kutosha kwa kivuko hiki
kulingana na idadi ya watu waliopo, hata hivyo kuna vivuko viwili ambavyo
hupishana kwa zamu.
Mwonekano wa eneo la Kando ya Ziwa Victoria.
No comments:
Post a Comment