HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 11, 2012

CHEKA NA MZEE KITIME

Mdada aliyekuwa anaishi na jamaa kinyemela alimng'ang'ania jamaa kama akidai keshapotezewa sana muda lazima jamaa amuoe. Kila ujanja jamaa aliofanya mdada kakaza kamba lazima aolewe.

Jamaa akaskuti, akapata jibu. Kaingia facebook kachagua picha za wadada wanne akaziprint, kisha kwenye kila picha akaandika RIP, akaficha kwenye kitabu akakiweka juu ya TV.

Mdada wakati wa kupukuta vumbi akazikuta zile picha akaziangalia akabaki na maswali.

Jioni jamaa aliporudi swali la kwanza likaanza;

MDADA: Samahani nimezikuta picha za wanawake kwenye kitabu ni akina nani?

JAMAA: Achana na zile picha

MDADA: Zinanishangaza kuna nini?

JAMAA: Niwe mkweli hebu leta hizo picha, huyu wa kwanza anaitwa Jeni, nilitaka kumuoa wiki mbili kabla ya harusi akagongwa na daladala, huyu mwingine Sara tulikutana kwenye pati ya kazini tukapenda siku ya kupeleka posa kwao majambazi wakaingia kwao na kuuwa watu wawili yeye akiwa moja wapo.

Huyu Davidina, alikuwa ndio kwanza katoka kusoma Ulaya shangazi yangu akanitambulisha tukapendana sana, wajomba wakapeleka posa kwao wakakuta msiba, aliangukiwa na ukuta wa nyumba iliyokuwa inajengwa akafa, huyu wa mwisho Esther ndie aliyekuwa mpenzi wangu wa mwisho kabla ya wewe, tulikuwa karibu tufunge ndoa baba yake akampa pesa aende Dubai, ndege yao ikaangukia baharini mwili wake haujaonekana, nilikaa kitambo nikitafakari hii mikosi kabla ya kuoa lakini nimeona ilikuwa bahati mbaya tu, ndio tukaonana na wewe.

Na kiukweli nimeamua lazima nipeleke posa kwenu kesho

MDADA: Posa sawa hata mimi nataka ulete, lakini ungengoja kwanza kesho asubuhi ntaenda kuwaona wazazi, unajua sijawaona muda mrefu, nikae huko kidogo halafu ntakubonyeza lini ulete posa

JAMAA: Sawa lakini usichelewe sana 

1 comment:

  1. HUYU MZEE KWA STORI KIBOKO, SIKOSAGI KILA ASUBUHI KUFUNGUA BLOG YAKE

    ReplyDelete

Post Bottom Ad