Asia dachi ambae ndiye mwanamitindo anaeshikilia taji UNIQUE MODEL baada kuvikwa mwaka 2010 ametoa wito kwa wasichana wenye vipaji vya uanamitindo kujitokeza kwa wingi siku ya leo kwaajili ya usaili wa kujiunga na shindano hilo.
Pia amewaomba wabunifu wa mitindo ya nguo kujitokeza kuwavalisha wanamitindo watakaokuwa wamechaguliwa kwani kwakufanya hivyo watapata nafasi ya kujitangaza na kuunga mkono harakati za ukuaji wa sanaa ya mitindo nchini Tanzania.
Ushirikiano mzuri umeonyeshwa na wabunifu nguli kama Asia Idarus na Gabriel Molel kwa kujitokeza na kuunga mkono harakati hizi za unique model 2012 ambapo inategemewa kuwa chombo pekee cha kukuza sanaa ya wanamitindo wachanga nchini Tanzania.
Usaili huo unafanyika leo tarehe 18 novemba katika hoteli ya Lamada iliyopo Ilala msimbazi center kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa saba mchana.
Giraffe ocean view hotel,Dtv,Gazeti la Tanzania Daima,mashujaa Investment ltd,
Sophernner Investment co,Fabak fashions,ltd,K.d.surelia,young don records,Kiu investment ltd,Michuzi blog,Oriental bureau de change,,88.4 clouds fm,J’s professional ltd,Lamada apartments hotel,Jiachie blog,Mtaa kwa Mtaa blog na Unique entertainment blog.
No comments:
Post a Comment