Mwalimu wa nadharia na Gitaa Abeid Mussa akiwaelekeza wanafunzi namna ya kupangilia muziki wakati wa kufanya onyesho
Wanafunzi wa mafunzo ya muziki wakiwa kwenye somo la matumizi ya viungo vya mwili katika kutengeneza midundo, yaani “body percussion’ picha zote na AMTZ.
Action Music Tanzania (AMTZ) ni asasi iliyosajiliwa na BASATA na kupewa namba ya usajili BST/4733, imeanza kutoa mafunzo ya upigaji ala za muziki kwa watu mbalimbali katika kipindi hiki cha likizo, yanayoitwa ‘Music December 2012’
Mafunzo hayo ya upigaji wa ala za muziki ni kwa watu wote ambao hawajaingia na wale waliokwishaingia katika tasnia ya muziki lengo likiwa ni kuwafundisha na kuwajengea uwezo kimuziki (muziki kama taaluma), ambapo mwanamuziki atajengewa uwezo wa kutunga, kuandika, kusoma na kucheza ala kitaalam na jukwaani yaani ‘Live’.
Mafunzo haya yanafanyika kuanzia mwezi disemba ili kutoa fursa kwa wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi na sekondari kujiunga, pia kuwapa nafasi watu walioko makazini kutumia fursa hii kujifunza muziki.
Mafunzo ya upigaji ala za muziki kwa vitendo yatahusisha ala za muziki kama Kinanda (piano,keyboard), Ngoma aina ya Konga, djembe na za mapipa, Tarumbeta ya Bb, Saxophone ya Eb (alto sax), Gitaa la sauti ya juu (solo, rhythm) na chini (bass), Seti ya Ngoma za Kimagharibi (drum set/kit) na Matumizi ya viungo vya mwili katika kutengeneza midundo, yaani “body percussion’.
Mafunzo hayo yataambatana na nadharia ya Music ambapo mwanafunzi atajifunza namna ya kuandika, kusoma na usikivu yaani ‘music writing, sight reading and ear training’.
Mafunzo yanafanyika katika ofisi za Action Music Tanzania Mwenge, maeneo ya ITV, karibu na Maryland bar – Shule ya Msingi Mwenge na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonyesho (FPA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mafunzo yanatolewa na walimu wa muziki kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma na kutoka kwenye bendi na taaisis nyingine za muziki hapa nchini.
Fomu za usajili zinapatikana ofisi ya AMTZ karibu na Shule ya msingi Mwenge kwa shilingi za kitanzania 2,000/= tu. Njoo ujifunze kupiga ala za muziki kwa muda mfupi na kwa bei nafuu.
Imetolewa na
Mandolin Kahindi
Katibu Mtendaji-AMTZ
CHUO HICHO KINAENDEA AU KILIISHIA MWAKA HUO TU NA KAMA KINAENDELEA NAOMBA NAMBA YA MAWASILIANO
ReplyDeleteKwa Dodoma Hamna kituo??
ReplyDeleteKAMA MAFUNZO YANAENDELEA NAOMBA PIA MAWASILIANO...
ReplyDeleteAda kiasi gani???
ReplyDelete