HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 30, 2012

WAZIRI WA VIWANDA BIASHARA NA MASOKO Dkt. ABDALLAH KIGODA AZINDUA TAWI JIPYA LA BENKI YA STANBIC

Waziri wa Viwanda ,Biahara na Masoko Dkt. Abdallah Kigoda akizindua tawi jipya la Benki ya Stanbic Kariakoo ambalo linakuwa la pili katika eneo hilo la Kariakoo sokoni jijini Dar es Salaam, mpaka sasa Stanbic inajumla ya matawi kumi na moja kwa nchi nzima .katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa benki hiyo Abdallah Singano(kushoto)Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa benki ya Stanbic Douglas Kamwendo 04. Waziri wa Viwanda ,Biahara na Masoko Dkt. Abdallah Kigoda akikalibishwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Douglas Kamwendo wakati wa hafala fupi ya uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya Stanbic Kariakoo ambalo linakuwa la pili katika eneo hilo la Kariakoo sokoni jijini Dar es Salaam, mpaka sasa Stanbic inajumla ya matawi kumi na moja kwa nchi nzima.Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa benki hiyo Abdallah Singano.
Waziri wa Viwanda ,Biahara na Masoko Dkt. Abdallah Kigoda akiagana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa benki ya Stanic Douglas Kamwendo baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo Kariakoo Sokoni.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Stanbic Tawali la Kariakoo sokoni wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika hafala ya uzinduzi wa tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt Abdala Kigoda amesema kuwa sasa ni wakati muafaka kwa benki zilizopo nchini kuwa wabunifu katika kuanzisha huduma za mikopo zitakazikidhi mahitaji ya wajasiriamali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la benki ya Stanbic lililopo Kariakoo jijini Dar es Salaam jana, waziri Kigoda alisema takwimu zinaonyesha kuwa benki nyingi zimekuwa zikitoa mikopo kwa wafanyabiashara wa kuuza na kununua na kuwasahau wale wanaowekeza katika uzalishaji

"Ninayo furaha kusikia kuwa benki ya Stanbic inayo huduma maalum kwa wajasiriamali ijulikanayo kama SME Quick loan ambayo nimeambiwa ni moja ya huduma zilizopokelewa vizuri sana na wateja na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa. Huduma hii ni nzuri kwa vile mteja kupata mkopo ndani ya saa 48

Wizara inatambua mchango wenu na kuwapongeza kwa jitihada zenu za kuinua wafanya biashara wadogo wadogo na wa kati. Napenda kutoa wito kwa mabenki mengine kuiga mfano huu endelevu," alisema

Akisoma hotuba kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki ya Stanbic, mkuu wa kitengo cha masoko wa benki hiyo Abdala Singano alisema kuwa tawi jipya la Kariakoo ni tawi na moja la benki hiyo hapa nchini

"Dhamira yetu si to kufungua matawi hapa Tanzania na kusonga mbele kwa benki bali ni kusonga mbele kimaendeleo pamoja na wateja wetu. Kariakoo ni eneo lenye wafanyabiashara wengi kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania pamoja na wageni kutoka nchi jirani za Burundi, Rwanda, Kongo, Zambia na Malawi.

Madhumuni letu kuu kama benki ni kuweza kuleta huduma zetu karibu na wafanyabiashara wadogo na wakati ambao wengi wao wapo hapa Kariakoo," alisema

Singano aliongeza kuwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ni muhimu katika kukuza na kuendesha uchumi wan chi yetu pamoja na kutoa ajira na kuongeza kuwa benki yake itaendelea kubuni huduma zitakazoweza kulinyanyua kundi hilo muhimu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad