HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 11, 2012

WAREMBO WA REDD'S MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO

Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2012 wakiwa nje ya jengo la Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro walikofika kujionea vivutio mbalimbali katika bonde la hifadhi hiyo ambalo lina mambo mengi ya ajabu miongoni mwa hifadhi. Mbali na kujionea wanyama wa aina mbalimbali na ndege pia warembo hao walipata fursa ya kujifunza juu ya Bonde hilo ambalo lipo katika mchakato wa kuingia katika Maajabu ya dunia.
Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja na Watalii waliofika katika Bonde la Ngorongoro kujionea vivutio mbali mbali.
Baadhi ya warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2012 wakipewa maelezo juu ya picha mbalimbali za Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro, wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo kwa kujifunza na kujionea mambo mbalimbali. Warembo hao wa Redd's Miss Tanzania 2012 wapo Kanda ya Kaskazini kwa ziara ya kuhamasisha Utalii wa Ndani.
Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakiwa pamoja na Watalii wengine wakioangalia maajabu ya Bonde la Ngorongoro ambalo ni moja ya vivutio vinavyotarajiwa kuingia kwenye maajabu ya Dunia.
Warembo wa Redd's Miss Tanzania Wakiwa kwenye Magari Maalum wakati wakiizungukia maeneo ya Bonde la Ngorongoro kujionea wanyama na ndege aina mbali mbali.
Warembo wakifurahia kutembelea hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.

2 comments:

  1. mei naombeni niulize kwanza haya mashindano yanayoendelea wkt huu na wakati miss world ilishafanyika na amepatikana ni ya nn maana tumezoea huwa yanafanyika kumtafuta miss tanzania ili akashiriki miss world sasa imekuwa kinyumeeee ndio hapo wanapotuchanganyaaaa ufafanuzi plz kwa anaelewa.

    impostra

    ReplyDelete
  2. Nikweli mashindano ya kumtafuta mrembo wa dunia yalishafanyika na mshindi alishapatikana na tanzania iliwakilishwa na mrembo wake nadhani kama sijakosea aliingia ktk tano bora akiwaacha nyuma warembo wengine kutoka nchi za afrika.Hao warembo uwaonao hapo kaka wapo ktk mchakato wa mwanzo wa mrembo wa dunia kwa fainali za mwakani hivyo basi ktk hao uwaonao hapo atachaguliwa mmoja wa kutuwakilisha ktk fainali zijazo za mrembo wa dunia nadhani kwa maelezo haya utakua ushapata picha halisia.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad