Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza akizungumza na Wahariri Watendajio wa
vyombo vya habari nchini (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam ikiwa ni
sehemu ya utaratibu aliojiwekea wa kukutana nao kupitua Jukwaa la Wahahriri kubadilishana
uzoefu juu ya shughuli za Vodacom hapa nchini.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Absalom Kibanda akiongea katika mkutano wa pamoja
kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
ya Vodacom Tanzania Rene Meza na wahariri Watendaji wa Vyombo vya Habari nchini
uliofanyika leo jijini Dar es salaam. Kupitia Mkutano huo Rene (kushoto) aliwaelezea
wahariri hao uwekezaji wa Vodacom katika huduma za mawasiliano na maendeleo ya
jamii kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Kampuni
ya Mawasiliano ya Vodacom imesema itaendelea kutoa kipaumbele katika
kusaidia huduma za jamii nchini kama shemu ya dira ya biashara ya
kampuni hiyo.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw Rene Meza
alipokutana na Wahariri Wakuu wa vyombo vya habari nchini jijini Dar es
salaam ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kuzungumza na wakuu hao wa
vyumba vya habari kwa lengo la kuzungumzia shughuli za Vodacom hapa
nchini.
Amesema
katika kuendeleza azma hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania kwa mwaka huu
wa fedha imetenga shilingi bilioni mbili na nusu kufadhili miradi
mbalimbali ya kijamii katika maeno makuu manne elimu,afya, mazingira na
uwezeshaji kiuchumi wanawake.
Rene
amesema mafanikio ya kibishara ya Vodacom hupimwa sanjari na namna
inavyowekeza katika jamii kupitia kitengo chake cha Vodacom Foundation
jambo ambalo linaifanya kambpuni hiyo kuwa karibu zaidi na jamii.
Amesema
mafanikio ya uwekezaji wake katika jamii – CSR yameonesha mafanikio
makubwa kupitia miradi mbalimbali ukiwemo wa fistula ambao umeleta staha
na faraja kwa wanawake waliokuwa wakisumbumuliwa na tatizo hilo na
mradi wa MWEI.
Akizungumzia
huduma ya M-pesa Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema Vodacom itaendelea
kuwa makini kuhakikisha mfumo wa huduma hiyo unaendelea kuwa imara na wa
kuaminika sokoni ikitambua nafasi iliyonayo katika kupunguza tatizo la
upatiakanji wa huduma za kibenki nchini.
Rene
amesema ni jambo la wazi kwamba huduma ya M-pesa imekuwa nguzo muhimu
katika maisha ya watu kwa sasa ikitoa urahisi wa kutuma na kupokea fedha
wakati wowote mahali popote hapa nchini kuzindi hata kupitia mifumo ya
kibenki.
Miamala
yenye thamani ya kiasi cha shilingi bilioni moja hupita katika mfumo wa
M-pesa kwa siku kutuma na kupokea pesa pamoja na kufanya malipo
mbalimbali.
Kuhusu
huduma za mawasiliano Rene amewaeleza wahariri kwamba kampuni hiyo
kupitia mpango wake wa kuporesha na kupanua upatikanaji wa huduma
itakamilisha mpango wa kujiunga na mkongo wa taifa kwa sehemu kubwa ya
nchi ifikapo Mei mwakani.
Akizungumza
katika mkutano huo Mwenyekiti wa jukwaa la Wahariri nchini Bw Absalom
Kibanda alisema uamuzi wa Rene kukutana na wahariri kila mwaka unajenga
imani na ukaribu kati ya kampuni hiyo na vyombo vya habari tofauti na
wakuu wengi wa makampuni binafsi ambao hawana utamaduni wa kudumu wa
aina hiyo.
Rene
aliyejiunga na Vodacom Tanzania Oktoba mwaka jana alikutana kwa mara ya
kwanza na Wahariri Wakuu wa Habari Novemba mwaka jana ambapo
aliwaelezea dira na mikakati yake ya kuhakikisha Vodacom inaendelea
kuongoza soko la huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini.



No comments:
Post a Comment