HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 15, 2012

Wadau tumsaidie dada huyu


Historia ya kweli kuhusu ndugu yetu Upendo Andrew,siku tatu kabla hajatoka masasi girls alipokuwa amemaliza shule, alitumbukia kwenye shimo lililokuwa likiwaka moto wa majani makavu ya mwembe, alizama hadi kufikia karibu ya kiuno.

 moto ulikuwa kama umechokolewa na kijiti alipotumbukia, alipelekwa mkomaindo, na baadaye miguu yake yote miwili ilikatwa, wazazi wake wote wawili walifariki kabla hatujamaliza shule, baada ya hapo alikuwa analelewa na babu yake, naye alikuja kufariki so alikosa msaada kabisa akaamua kwenda dar ambapo hakuwa na ndugu, hivyo akaanza kazi ya omba omba.

kama tulivyosikia toka kwa wadau huwa anaomba imala seko na maeneo mengine ya katikati ya mji, alipata mtu wa kumsomesha compyuta, akapata kazi, lakini kila akikaa ofisini machozi yanatoka tu hivyo kazi ikashindikana. aliambiwa na doctor wa hospital ya mission ndanda kuwa kuna mshipa umefail kichwani ndo unasababisha hayo.

Kwa maana hiyo alishauriwa kutumia vitamin B, wiki moja kila mwezi, maisha yake yakawa kimtindo huo, amepanga kigamboni, leo nimempigia simu bahati nzuri ana simu na anapatikana, Mungu ni wa maajabu, upendo ana mtoto mdogo wa miezi mitatu, anaishi vipi sasa, mtu aliyemzalisha anafanya kazi za ndani kwa wahindi, ana mke na watoto wawili, hapa tunaona kabisa anahitaji msaada mkubwa kutoka kwetu sisi sote, kwani hata shughuli ya kuomba imesimama kutokana na mtoto ni mdogo, namba yake ni 0715271201.

 katika zungukazunguka yangu na baadhi ya mawazo kutoka kwa watu kwamba je tumsaidieje kwa kitu cha kudumu, nilimpigia ili kupata mawazo toka kwake, tuliongea sana akasema basi kama inawezekana akipata computer na photocopy machine na chuma cha kufanyia biashara hiyo, anaweza kufanya, sasa wapendwa hebu tujitoeni kwa moyo tufanye tunaloweza ili kumsaidia, kwa yeyote aliyeguswa either unamfahamu ama humfahamu, lakini taarifa yake ndo hiyo hapo, amesoma shule ya msingi Ligula iliyoko mkoani Mtwara na baadae kwenda secondary Masasi Girls.

Kama umecheza naye hukucheza naye sote ni binadamu sote ni ndugu, kwa aliyeguswa jamani,Namba ya mpokeaji wa michango ni 0754463508,MRS Anneth Makunga Ghullam, pia mnaweza kuwasiliana na @violet mkapa on 0754574421 kwa sababu yeye alishawahi kukutana naye ana kwa ana.

Mchango wako unaweza kufanikisha jambo zima la kumkwamua Dada huyu mwenye kuhitaji sana msaada wako,kama Mtanzania au mwanadamu yoyote mwenye roho ya huruma. 

 Msaada unaohitajika: 

Wadau baada ya kupata historia fupi ya Upendo,msaada unaohitajika ni wakufanya mpango ili afunguliwe biashara na imekadiliwa milioni mbili ingeweza kusaidia kufungua biashara hiyo ,mpaka sasa pesa iliyopatikana ni 460.000,hapo wadau ni mbali mpaka kufikia milioni mbili tu na ndio maana tunaomba wadau wa sehemu mbalimbali toka mahali popote waweze kutusaidia kufanikisha jambo hili.

Kutoa ni moja na pamoja tunaweza fanikisha swala hili zima.Unaweza kujiunga kwenye kundi hili la kumsaidia upendo kwa Facebook kwa kufuata link hii hapa http://www.facebook.com/groups/184474061657697/.  

1 comment:

  1. kwanza kabisa namuomba mmiliki wa hii page na mtoa mada arekebishe namba ya simu ya Violet Mkapa ni 0754571121

    ReplyDelete

Post Bottom Ad