Meneja
wa huduma za jamii wa Vodacom Foundation Mwamvua Mlangwa, akikabidhi
mfano wa hundi ya fedha kiasi cha shilingi Milioni 20, kwa Mkurugenzi wa
kituo cha Tanzania Mitindo House, Khadija Mwanamboka, Kwa ajili ya
kuanzisha chuo cha mafunzo ya Mitindo kwa Watoto yatima.
Zaidi
ya watoto yatima 50 waishio katika mazingira magumu watapata mafunzo ya
ubunifu wa mavazi. Hii inafuatia kuanzikwa kwa kwa kituo cha ubunifu wa
mavazi , (Mitindo House) kitakachokuwa chini ya Mwanamitindo maarufu,
Hadija Mwanamboka.
Kituo
hicho kitatoa mafunzo ya ushonaji, ubunifu wa mavazi, na utengenezaji
wa vito mbalimbali kimefadhiliwa na mfuko wa huduma za jamii wa Vodacom
(Vodacom Foundation)
Akizungumza baada ya kupokea mfano wa hundi ya shilingi Milioni
Ishirini, Mkurugenzi wa kituo hicho, Hadija Mwanamboka, amesema kuwa
lengo lao ni kuwawezesha watoto yatima waishio katika mazingira magumu
na wasio na elimu kuweza kujitegemea kwa kujiajiri wenyewe kutokana na
ujuzi watakao upata.
“Tutatoa
mafunzo kwa watoto wanaoishi katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto
yatima, yatakayo wawezesha kupata fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika
majukwaa ya sanaa na baadae kuwawezesha kujiajiri wao wenywe.”
“Mafunzo
haya yatatolewa kwa mwaka mzima, wanafunzi ishirini na tano watapata
mafunzo ya ushonaji na ubunifu wa mavazi na wengine 25 watapata mafuzno
ya uchongaji wa vito mbalimbali na uchoraji,” alisema Hadija.
Kwa
upande wake, Meneja wa Huduma za jamii wa Vodacom Foundation, Mwamvua
Mlangwa amesema kuwa Vodacom Foundation imedhamiria kuboresha maisha ya
jamii ya watanzania wanaoishi katika mazingira magumu.
“Vodacom
Foundation itaendelea kuwaunga mkono watanzania hususani wale wanaoishi
katika mazingira magumu kwa kuwasaidia kujenga maisha yao na kusaidia
kukua kwa uchumi wa nchi kupitia mipango mbalimbali tuliyonayo katika
kitengo chetu,” alisema Mlangwa.
No comments:
Post a Comment