Mrembo
wa Ilala, Magdalena Roy, usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kunyakua taji
la mrembo wa pili kuingia hatua ya nusu fainali ya Redd's Miss Tanzania
2012 baada ya kuwashinda warembo wengine 29 na kutwaa taji la Top
Model.
Magdalena
aliibuka mshindi katika shindano dogo la Redd's Miss Tanzania
lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Kimataifa ya Naura
Springs jijini Arusha.
Kwa
matokeo hayo Top Model, Magadalena Roy anaungana na Miss Photogenic,
Lucy Stephano katika nusu fainali hiyo na kukaa tayari kusubiri warembo
wengine 13 watakaoungana katika Nusu fainali hizo.
Taji la TOP MODEL lilikuwa linashikiliwa na mrembo wa Temeke, Mwajabu Juma.
Mrembo
kutoka Mkoa wa Mara na Miss Kanda ya Ziwa 2012, Eugene Fabian nae
alifanikiwa kutwaa taji la Ubalozi wa Hotel ya Naura Spring ya jijini
Arusha.
Egene
alitangazwa kunyakua taji hilo usiku wa kuamkia leo wakati wa shindano
dogo la Redds Miss Tanzania 2012 la kumsaka Top Model ambaye pia
ataingia katika hatua ya 15 bora ya Shindano hilo la taifa la Miss
Tanzania. Awali taji la Balozi wa Naura Spring Hotel lilikuwa
likishikiliwa na Neema Joel.
Warembo walioingia hatua ya tano bora ya Top Model Redd's Miss Tanzania 2012.
Washiriki wa Shindano dogo la kumtafuta Top Model wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakipita jukwaani kuonyesha mavazi mbali mbali.
MC Mpoki akiimba sambamba na Mwanamuzi Linah a.k.a Ndege Mnana.
Sam wa Ukweli akifanya vitu vyake.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Sam wa Ukweli akiwa amenyanyuliwa juu juu na Wacheza shoo wake.
Dogo anaecheza kwa kumuigiza Michael Jackson akionyesha uwezo wake stejini.
Majaji wakipitia majina ya washiriki na kujadiliana.
Wadau wa TBL Arusha.

Wadau wa Habari wa Jijini Arusha,Kulia ni Woinde Shizza wa Globu ya Jamii.
Wakubwa wakijadiliana jambo.
Miss Tanzania anaeshikilia taji hivi sasa,Salha Israel (kulia) akiwa na aliekuwa Matron wake.
Wadau wa Radio 5 ya jijini Arusha.
Meza kuu.
Wadau
mbali mbali wa jijini Arusha walijitokeza kwa wingi kwenye ukumbi wa
Hoteli ya Naura Springs kushuhudia anavyopatikana Top Model wa Redd's
Miss Tanzania.
Mdau Alex (kushoto) na Angel Justice wakiwa kwenye picha ya pamoja na Msanii Linah.
Wadau B.12 na Babuu wa Kitaa nao hawakucheza mbali na shoo hiyo.
Mdau Alex (kushoto) na Angel Justice wakiwa kwenye picha ya pamoja na Msanii Linah.
Wadau B.12 na Babuu wa Kitaa nao hawakucheza mbali na shoo hiyo.

No comments:
Post a Comment