Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini,Sheikh
Issa Ponda (katikati) akiwa na wenzake 38 kwenye Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mapema leo walipofika kusomewa mastaka
ya makosa yao mbali mbali yakiwemo ya uchochezi wa kidini.Katibu amepandishwa
kizimbani leo pamoja na wenzake 50 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuwashawishi baadhi ya Waislamu kuvamia Kiwanja katika eneo la
Chang'ombe jijini Dar es Salaam,
kuwashawishi Waislamu kutojitokeza katika zoezi la Uandikishaji katika
Sensa ya Watu na Makazi.
Baadhi ya Kina Mama wanaounganishwa na Mashtaka hayo pamoja na Sheikh Ponda,wakijificha ili wasipigwe picha wakati wakiwa kwenye chumba cha Mahakama leo.
Wanahabari wakitafuta taswiza za Sheikh Ponda wakati akiondolewa Mahakamani hapo.






Vurugu hizi zinasababishwa na DHULMA KUBWA inayofanywa na baadhi ya Wakristo walioko madarakani (wengi wao) kwa kusaidiana na baadhi ya Waislam walioko vile vile madarakani (wachache wao). Wote hao kwa pamoja, tena kwa makusudi kabisa na chini ya mikakati yao endeleveu, wanaukandamiza Uislam na wanawanyima Waislam haki zao za kimsingi kana kwamba taifa hili ni la Wakristo tu pekeyao. Walioko madarakani watumie BUSARA NJEMA ya kuacha dhulma hiyo badala yake wawape Waislam nao haki zao ambazo sasa zinafahamika kuanzia A mpaka Z badala ya kusubiria hadi tuuane kama walivyouana Warundi na Warwanda ambao mauanaji yao yalikuwa ya kikabila wakati yetu sisi Watanzania yatakuwa ya kidini ambayo yote hayo kwa pamoja suluhu zake huwa hazipatikani kirahisi na huchukua miaka mingi sana mpaka baada ya watu kwishauana malaki kwa malaki kama si mamilioni kwa mamilioni.
ReplyDelete