BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ imetoa ratiba yao katika wiki.
Baada ya kutoa burudani Dar es salaam wiki iliyopita sasa wamerudi tena kwa ajiri ya kutoa burudani nzuri zaidi wamesema kuwa wataanza kutoa burudani
Siku ya Jumatano ambapo watakuwa ndani ya Ashok Pub-Mbagala Kuu, Alhamia watakuwa Ya Wipes Pub-Mivinjeni, Ijuma watakuwa katika bonanza,Lidaz Club-Kinondoni,Jumamosi Hii Watakuwa Kigamboni katika Ukumbi wa Mama'Z & Papa'Z. na jumapili watamaliza wiki end katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni
Akiongea na Mtandao huu,Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa wameamua kutoa ratiba hiyo ili mashabiki wao waweze kujua nini kinachoendelea baada ya kumalizika kwa wiki iliyopita .
“Msondo ipo kamili katika kutoa burudan na ndiyo maana imeamua kutoa ratiba, hivyo tunaamini mashabiki wetu watakuja kwenye maonesho yetu kwani bila wao sisi hatuwezi kusimama na kuimba,” alisema Super D.
Alitaja vibao vinavyotamba kwa sasa vya bendi hiyo kuwa na Suluhu wa Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga mbali na nyimbo hizo bendi hiyo itapiga nyimbo zake zilizotamba zamani zikiwemo Asha Mwanasefu,Cheusi Mangara,mwana Mkiwa na nyingine nyingi zilizotamba kipindi hicho
No comments:
Post a Comment