HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 31, 2012

Mgambo wa Jiji na Zoezi la Kuwaondoa Wamachinga katikati ya Jiji la Dar


Mgambo wa Jiji la Dar es Salaam mchana wa leo wameendesha zoezi lao la kuwaondoa wafanya biashara ndogo ndogo (maarufu kama wamachinga) maeneo ya katikati ya jiji,hali hii imeleta  malalamiko mengi kutoka kwa wafanya biashara hao, ambao wamilalamikia kwamba wanaonewa,kwani wao wameamua kujitafutia riziki kihalali katika maeneo yasiyo rasmi kwa mujibu wa halmashauri ya jiji la Dar. Ila Wafanya Biashara hao wamelalamikia utaratibu unaotumiwa na Mgambo hao wa kukamata biashara zao na kwenda nazo wanakokujua wao.
Mgambo wa Jiji wakipakia kwenye Gari vifaa mbali mbali vinavyotumiwa na Wamachinga hao.
Wakiendelea na zoezi lao.
Vifaa vikiendelea kupakiwa kwenye magari.
Mmoja wa Mgambo hao akizungumza na Mmachinga alichukuliwa bidhaa zake.

1 comment:

  1. Huo ni uonevu na dhulma ya hali ya juu!sasa hao wanamgambo wanataka wananchi wakaibe?Hayo ndiyo yaliyotokea Tunisia hadi wananchi siku moja walichoka na kumtimua Rais na serikali yake!Na hata Tanzania watu siku moja watakuja kuchoka mambo ya uonevu na dhulma wanavyofanyiwa!Kwani serikali inashindwa nini kuwatengea wamachinga sehemu yao ya biashara wanayoipenda wao?Kuliko serikali kuwachagulia sehemu isiyokuwa na biashara!

    ReplyDelete

Post Bottom Ad