Watu
8 wamefariki dunia papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya
akiwemo Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya,Mh. Mary Mwanjelwa baada ya
lori la mafuta lenye nambari za usajili T81 4BTC na tela lenye namba
T815 BTC lililokuwa likitelemka katika mlima wa Iwambi Mji wa Mbalizi
kufeli breki na kwenda kuyagonga magari matatu ambapo kati ya hayo
magari mawili yaliteketea kwa moto.
Lori
lililosababisha ajali hiyo likiendelea kuteketea kwa moto.
Ripota wa habari hii kutoka jijini Mbeye anaendelea kutupasha kuwa ndani
ya gari la Mbunge huyo kulikuwepo na watu wawili ambapo dereva wa gari
hilo alijeruhiwa miguuni na kichwani huku mwanamke mmoja anayesadikiwa
kuwa Katibu wa Mbunge huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja
inadaiwa kuwa ameteketea kwa moto.
Akizungumza
na waandishi kwenye eneo la tukio,Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abass Kandoro
alisema ajali hiyo imetokea kwa magari manne ambapo kati yao matatu
yameteketea kwa moto papo hapo likiwemo gari la Mbunge Toyota Hilux.
Alisema, gari lingine lililoteketea kwa moto ni gari ndogo ya abiria
aina ya Toyota Hiace yenye namba T587 AHT ambalo lilikuwa na watu kumi
ambao kati yao wapo waliofariki na kujeruhiwa na lori lenyewe la mafuta
limeteketea kwa moto.
Akizungumzia
tukio hilo kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alisema
baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ni Mbunge Mary Mwanjelwa ambaye
anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Teule ya Ifisi baada ya
kuumia kwenye kiuno na dereva wake ambaye ameumia miguu na kupata
majeraha kichwani.
Majeruhi
wengine wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali Teule ya Ifisi
na wengine hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na kwamba hali ya Mbunge
inaendelea vizuri.
Ripota wa habari hizi alizungumza na baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo
ambao walisema kuwa Lori hilo la mafuta lilikuwa likishusha mlima huo wa
Iwambi, huku mbele yake kukiwa na Lori lingine la mizigo ambapo dereva
wa gari hiyo alifanikiwa kulipisha Lori hilo na ndipo lilipoyagonga
magari hayo mawili ambayo mbali na kupinduka kandokando ya barabara pia
yaliteketea kwa moto.
“Lori
la mafuta lilikuwa katika mwendokasi na ndipo lilipoligonga lori
lingine la mizigo na kisha kwenda kuyagonga magari madogo mawili na
kusababisha ajali hiyo kutokea,”alisema Alisi Mwakisapi.
Alisema, Mbunge wa viti maalumu aliokolewa na bodaboda iliyokuwa karibu
na eneo hilo kwa kile alichokidai kuwa mara baada ya kufanikiwa kutoka
ndani ya gari hilo dereva huyo alimuona na kumchukua kwenye bodaboda na
kumuwahisha hospitali.
“Katika gari alilokuwa amepanda Mbunge, alikuwemo dereva na mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuteketea kwa moto,”alisema
Hata
hivyo, miili ya marehemu tisa imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya
Mkoa wa Mbeya na hospitali Teule ya Ifisi majina yao hayajatambuliwa na
kwamba mwili wa mwanamke mmoja ambaye alikuwa kwenye gari ya Mbunge
uliteketea kwa moto.
Baadhi ya maiti zikiwa zimehifadhiwa sehemu moja kabla ya kupelekwa hospitali.
![]() | |||
Mkuu wa mkoa Mbeya,Abas Kandoro akiangalia ajali iliyotokea mbalizi mbeya mchana wa leo |
No comments:
Post a Comment