HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 16, 2012

Yanga na Prison ya Mbeya hakuna mbabe

Kikosi cha Yanga.
Kikosi cha Prisons.
 Mshambuliaji Machachari wa timu ya Yanga,Said Bahanuz akijaribu kutaka kumtoka mlinzi wa timu ya Tanzania Prison ya Jijini Mbeya,Lugano Mwangama wakati wa Mchezo wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye uwanja wa Sokoine,jijini Mbeya.katika mchezo huo wa leo,hakuna timu yeyote iliyofanikiwa  kuzifumalia nyavu za mwingine na kufanya matokeo kuwa 0-0.timu ya Yanga ni moja ya timu zinazodhaminiwa ni Bia wa Kilimanjaro Premium Lager.
 Mlinzi wa timu ya Tanzania Prison ya Jijini Mbeya,Lugano Mwangama akiwania mpira na kiungo wa Yanga,Haroun Niyonzima wakati wa Mchezo wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye uwanja wa Sokoine,jijini Mbeya.
 Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Said Bahanuz akitakata katikati ya walinzi wa timu ya Prison ya Mbeya leo.
 Heka heka langoni mwa timu ya Prison lakini haikuzaa matunda.
 Mshambuliani wa Yanga,Hamis Kiiza akichuana na Mabeki wa Prison ya Mbeya.
 Hapa ni kupimana msuli tuuu.....
 ya kipaaa.
 Hapiti mtu hapaaa...
Wadau wa huduma ya kwanza (sijui wanaitwaje).
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh. Abbas Kandoro akiwasili uwanjani.
Wazee wa Kazi,toka Shoto ni mie mwenyewe mzee wa Mtaa kwa Mtaa,Mdau Mwaisango wa Libenele la Mbeya Yetu pamoja na Rashid Mkwinda wa Fasihi za Ufasaha tukiwa ndani ya uwanja wa Sokoine jijini,Mbeya.
Mashabiki wa timu ya Prison ya Mbeya na shangwe ya droo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad