Habari ankal
Asante kwa kuniwekea habari zangu nyingi kuhusu Ugiriki
Licha ya baadhi ya watu kuona tunawabania kuja Ugiriki na kuuliza kwa nini nyie mpo kama kuna matatizo.
Ukweli
ni huu Chama cha XRISI AVGI au Golden down(Neo Nazi) kimeanza piga piga
ya wageni wakiongozwa na wabunge wao ambao polisi inashindwa kuingilia
kati wakiwepo.
Jana usiku wa kuamkia tar 26 ofisi za Jumuiya ya watanzania ziliharibiwa vibaya na baadhi ya watu kujeruhiwa.
Licha ya kuwepo kwa Polisi bado walishindwa kuzuia tukio hilo na kuonekana polisi wakiwapa mgongo kabisa Watanzania
baada ya hapo walielekea maeneo mengine ya mabaa ya wageni yaliyopo karibu na kuharibiwa vibaya pia.hizi ni
Baadhi tu ya picha na news pia zipo kwenye mitandao mingi tu.
Ahsante.
Mdau Umangani.
Baadhi ya Watanzania wakiwa nje ya Ofisi za Umoja huo huku wakiwa hawana la kufanya.




No comments:
Post a Comment