HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 18, 2012

WANYAMA AINA YA NYUMBU WAANZA KUREJEA SERENGETI WAKITOKEA VEKESHENI NCHI JIRANI

Watalii kutoa sehemu mbali mbali Duniani wakiongea na wanahabari kwa furaha baada ya kuona Wanyama aina ya Nyumbu wakirejea toka Vekesheni,nchi jirani.
Wanahabari wakichukua Matukio muhimu wakati msafara wa Nyumbu ukirejea toka vekesheni nchi jirani.
Huyu anaonekana kuelemewa na maji.
Msafara umekolea.

Na Woinde Shizza,Serengeti

Msafara maarufu duniani unaohusisha wanyama aina ya Nyumbu umeanza kurejea katika makazi yao ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakitokea mapumziko katika nchi ya jirani.

Kila mwaka, nyumbu pamoja na wanyama wengine kama pundamilia na swala hufanya mzunguko maalum unaochukua miezi 12 ya mwaka ambapo miezi kumi kati ya hiyo huwepo nchini katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na iliyobaki hutumiwa na wanyama hao katika eneo la Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya.

Mwaka huu msafara huu unaohusisha wanyama zaidi ya Milioni Moja na Nusu na ambao hutembea katika mzunguko wa takribani Kilometa 1,000 umewahi sana kurejea nchini ukitokea mapumziko nah ii kwa mujibu wa taarifa za kitaalamu inatokana na kuwahi kunyesha kwa mvua katika eneo la Serengeti ambapo imesababisha kuwepo na nyasi nzuri ambazo ni chakula muhimu kwa wanayama hawa.

Changamoto kubwa wanayokutana nayo msafara huu mara unaporejea nyumbani ni tukio la kuvuka Mto Mara ambao umejaa wanyama wakali aina ya mamba na viboko ambao nao huwa ni msimu wao wa kujipatia chakula kwa kuvizia na hatimaye kuwakamata wanyama hawa mara wanapovuka mto.

Watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekuwa wakifurika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushuhudia tukio hili adimu la kuvuka Mto Mara ambalo wengi wao wamekuwa wakiliona kupitia filamu mbalimbali zilizotengenezwa katika eneo hili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad